skip to main |
skip to sidebar

5/11/2012 05:34:00 PM

Unknown
No comments

BAADA ya kufanikiwa kurejea Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, timu ya
maafande wa Tanzania Prisons ya Mbeya, imeapa kutorudia makosa
yaliyoifanya ishuke daraja misimu miwili iliyopita na tayari imeanza
kujipanga kwa msimu ujao wa Ligi.
Msemaji wa idara ya michezo wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mrakibu
Mwandamizi (SSP), Elisha Kitojo, alisema kuwa, wamejifunza kwamba,
wanapaswa kufanya kila wawezalo kuhakikisha hawashuki daraja, kwa vile
Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu mno.
Alisema, ili timu iweze kufanya vema katika Ligi daraja la kwanza,
inapaswa kujipanga kutokana na timu kuwa nyingi na inapofikia hatua ya
tisa bora, kuna vikwazo vinavyotokana na mambo kadhaa, lakini tatizo
likiwa kwa timu mwenyeji kuwa na nafasi kubwa ya kupanda.
“Tanzania Prisons tunashukuru kwamba tumefanikiwa kurejea Ligi Kuu hivi
sasa, hatutakubali tena kushuka daraja kwa kuwa huko ni kugumu na
hakufai, ili kuhakikisha hayo hayatukuti tena, tunasubiri ripoti ya
mwenyekiti wa timu yetu ili tuanze kujipanga,” alisema Kitojo.
Alisema kuwa, wanasubiri kuipitia ripoti hiyo, ambayo ilitarajiwa
kuwafikia jana, hivyo wanaweza kuanza kuipitia kuanzia leo na baada ya
hapo wataanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao, ikiwa ni pamoja na
kufanya usajili na kisha kuanza mapema maandalizi ya Ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment