Mahitaji
- Maharage (beans 2 vikombe vya chai)
- Nazi (coconut milk kiasi)
- Vitunguu maji (onion 1kikubwa)
- Nyanya (fresh tomato 1)
- Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai)
- Chumvi (salt kiasi)
- Curry powder 1 kijiko cha chai
- Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Chemsha
maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka
vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka
nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko
uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache
lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa
0 comments:
Post a Comment