Bunjak kulia akiwa na Kali Ongala na Daktari wa timu katika mechi ya juzi dhidi ya Simba |
KOCHA
Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa
kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
Habari
kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa
Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa
ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak
anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne
tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na
kutoa sare tatu.
Bunjak
mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti
7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha
mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK
Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki
Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd,
Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali,
Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka
katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki
(Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK
Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart
alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu
hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia
huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu
ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos
Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini
Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya
kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili
katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki
na Kagame mwezi uliopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe
tena.
Stewart
ana sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake,
kwa mfano namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali
kama mchezaji, lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana
naye awe Kocha Msaidizi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga,
akakubali.
Chini
ya Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea
kujiamini zaidi na mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la
Urafiki, akaifikisha fainali, ambako ilifungwa na Simba kwa penalti
kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
0 comments:
Post a Comment