skip to main |
skip to sidebar

8/20/2013 08:04:00 AM

Unknown
No comments
Mchungaji Albogast baada ya kuachiwa huru.
Akikumbatiwa na mpendwa wake.
Wachungaji wengine wakirudishwa rumande kwa muda kusubiri hukumu.
Wakirudishwa rumande.
...Hapa wakati wakisubiri hukumu kizimbani.
Wakili wa washitakiwa, Atson Ndusyepo akiongea na wanahabari baada ya hukumu.
Umati
wa watu wakiwemo waliokuwa wateja wa Desi waliofika mahakamani hapo
kujua hatima ya fedha walizopanda wakitoka nje ya mahakama baada ya
kuambiwa hawana chao.
Wachungaji watano wa makanisa ya Pentekoste waliokuwa wakishikiliwa
kwa tuhuma za kuendesha biashara ya upatu kupitia Taasisi yao ya Desi
Tanzania na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu leo mmoja wao
aitwaye Albogast Francis ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia
wakati wengine wanne wakihukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa
faini ya shilingi milioni 21 kila mmoja pamoja na kutaifishwa mali zao.
Kesi hiyo ambayo imeunguruma kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar
takribani miaka minne, kupitia kwa hakimu wake, Aloyce Katemana ilitoa
hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa
utetezi na Jamhuri. Vilevile kwa wale wote waliopanda katika taasisi
hiyo wote wameonekana kutenda kosa, hivyo hawana chao.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)
0 comments:
Post a Comment