Nyota wa Simba, Emmanuel Okwi ameamua kurejea nchini na kujiunga na timu hiyo.Kurejea kwake kutakuwa faraja kubwa kwa Simba iliyokosa mshambuliaji wa uhakika kwenye michuano ya Kombe la Kagame. Hata hivyo, taarifa za kurudi kwake zimekuwa zikichanganya.Taarifa za awali, zinaonyesha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini alikofanya majaribio imeamua kumuacha pamoja na kuonyesha kiwango kizuri. Tatizo kubwa limeonekana ni nidhamu.Nyingine inaeleza ameamua kurejea Simba baada ya kutoridhishwa na mazingira ya Afrika Kusini, tofauti na alivyozoea Tanzania na Uganda.
Wakala Ivica Stankovic aliyempeleka, jana aliliambia Championi: “Nidhamu ni tatizo, siwezi kukubali abaki timu kubwa kama Kaizer Chiefs halafu kesho anisababishie matatizo, nimeona wacha aondoke tu.”
Hivi karibu Okwi aliwaweka madaktari wa Kaizer Chiefs waliokuwa wakimsubiri kwa zaidi ya saa mbili apimwe afya kabla ya kujiunga na timu hiyo.Lakini jana mmoja wa viongozi wa Simba alisema: “Okwi amesema anataka kurudi Simba, hivyo baada ya mapumziko nafikiri ataanza mazoezi na wenzake.”
Kaizer Chiefs ilikuwa tayari kutoa kitita cha zaidi ya dola 150,000 (zaidi ya Sh milioni 220) ili kumnasa mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kuichambua ngome ya timu yoyote ile.
0 comments:
Post a Comment