Wednesday, October 12, 2011

BASI LA SHABCO EXPRESS LAPATA AJALI ENEO LA MSAMBIAZI, KOROGWE

Basi la Shabco Express ambalo lilikuwa likieleka Arusha leo limepata ajali baada ya kupinduka katika kona za Msambiazi, Korogwe. Kwa mujibu wa abiria waliokuwa ndani ya basi hilo, walisema basi hilo lilipinduka baada ya kutaka kulikwepa gari dogo na kujikuta likitumbukia mtaloni kutokana  na hali ya mvua na ukungu uliokuwa umeenea barabara nzima. Hakuna mtu aliyekufa katika ajali hiyo.



0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine