Wednesday, October 12, 2011

JESHI la polisi mkoani Iringa limemkamata mwanahabari Jerry Muro (pichani) kwa tuhuma za kudaiwa kutaka kuwapiga picha askari wa kikosi cha usalama barabarani eneo la ukaguzi wa magari (check point) Igumbilo Manispaa ya Iringa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Donald Mashambara, alimeuthibitishia mtandao huu juu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo na kuwa hadi majira ya saa 10 za jioni jana alikuwa bado akihojiwa na polisi toka majira ya saa 5 asubuhi alipokamatwa.

Mashambara alisema kuwa sababu ya mwanahabari huyo kukamatwa ilitokana na hatua yake ya kudaiwa kuwapiga picha askari wa usalama barabarani wakati wakiwa kazini.

Alisema kuwa Muro alikamatwa majira ya saa 5 .30 asubuhi jana wakati akiwa safarini kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya.

Kaimu kamanda huyo alisema kuwa Muro ambaye alikuwa akisafiri na basi la Summry baada ya kufika katika eneo hilo la Igumbilo akiwa na wenzake wawili alishuka kwa madai kuwa basi hilo lilikuwa limejaza abiria na yeye kuamua kurudi hadi kituo cha ukaguzi cha Igumbilo na kuanza kupiga picha askari polisi kwa kutumia simu yake yenye kamera.

"Kutokana na hatua ya mwanahabari huyo kupiga picha askari ndipo walipoamua kumkamata na kumfikisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kujua sababu ya kuwapiga picha"

Alisema Mashambara kuwa baada ya mahojiano na upekuzi uliofanywa na polisi katika kamera ya mwanahabari huyo walibaini kuwa hakukuwa na picha yoyote ambayo ilikuwa imepigwa na hivyo kulazimika
kumwachia huru.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine