WASANII wa filamu Bongo, Catherine Rupia ‘Cathy’, Jacqueline Wolper na Jennifer Kyaka "Odam" juzi kati walijikuta wakimwaga machozi kufuatia kusikitishwa na hali aliyonayo msanii mkogwe wa fani hiyo, Saidi Fundi ‘Mzee Kipara’.
Tukio hilo lilijiri Oktoba 11, mwaka huu baada ya wasanii kadhaa wanaounda klabu ya wasanii ya Bongo Movie kumuibukia mzee huyo nyumbani kwake, Kigogo jijini Dar es Salaam kumjulia hali pamoja na kumpelekea msaada.
Wasanii waliokuwemo katika msafara huo ni pamoja na Steven Kanumba, Issa Mussa, Jacob Steven ‘JB’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Mahsein Awadh ‘Dk.Cheni na wengineo.
Wakiwa nyumbani hapo, wasanii hao walionesha kusikitishwa na hali aliyonayo mzee huyo, mazingira yaliyosababisha wengi wao kugubikwa na nyuso za simanzi na kuanza kulia.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa Kundi la Maigizo la Kaole Sanaa Group, Sam Mchoma ‘Chiki’ alisema kuwa wameguswa sana na hali aliyonayo mzee huyo, hivyo wengine wajitokeze kumsaidia.
“Tumeguswa sana na ugonjwa wa mzee wetu na ndiyo maana tumeamua kutoa hiki tulichonacho kama sehemu ya msaada wetu. Hata kama ni kidogo tunaamimi kitamsaidia,” alisema Chiki.
Mzee kipara anasumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu, hali inayomsababishia mgogoro kiafya na kumfanya ashindwe kutembea.
0 comments:
Post a Comment