Tuesday, November 29, 2011

ALPHA WA PROJECT FAME na uamuzi wa kuimba GOSPEL!

Alpha Rwirangira
Mshindi mara mbili wa shindano la tusker project fame Mrwanda ALPHA RWIRANGIRA, ameamplfy  wazi kuhusu uamuzi wake wa kuingia moja kwa moja kufanya muziki wa gospel na kuachana na muziki usio wa gospel anaoufanya sasa.
amesema “nimekuja kugundua kwamba nimeimba nyimbo nyingi zimekua hits kama SONGA MBELE na AY, zilipendwa lakini nimegundua kwamba yule ambae alinipa hiki kipaji sijamrudishia haki yake, yani MWENYEZI MUNGU, so nimeamua nimrudishie utukufu.
mimi kama mkristo acha nimshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea, na wala sio kwamba nimeamua kuimba gospel kwa sababu kwenye muziki huu mwingine ni kugumu, hapana, kwanza kwenye gospel ndio kugumu zaidi, hizi nyimbo za kawaida nazifanya kibiashara na nimeweza kupata tuzo kama za MUSEKE na PAM AWARDS, kama ingekua ngumu nisingefanikiwa” ameamplfy ALPHA
Rwirangira amemalizia kwamba maamuzi yake sio kwamba atakua anafanya muziki wa gospel moja kwa moja, atakua anaimba nyimbo za kuisaidia jamii, “labda next time nitakua na project ya kuisaidia somalia or something, mimi nimeokoka na wala sio karibuni ni toka siku nyingi na nilikua naimba kanisani” alimalizia

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine