Tuesday, December 20, 2011

Maskini Davina, atupwa segerea




MSANII wa filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’(pichani) Ijumaa iliyopita alijikuta akipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa Segerea kufuatia kesi iliyokuwa ikimkabili ya kuharibu mali za mzazi mwenzake (jina tunalihifadhi).
Davina alifika kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam akiwa na matumaini ya kurudi ‘home’ lakini baada ya kusomewa mashitaka na jitihada za kuwekewa dhamana kukwama, amri ilitolewa ya yeye kupelekwa rumande hadi kesi yake itakapotajwa tena.
Baada ya amri hiyo, gazeti hili lilimshuhudia msanii huyo akiishiwa nguvu na hata wakati akipanda kwenye karandinga alionekana kukosa amani kitendo kilichowasikitisha baadhi ya wasanii wenzake waliokuwa mahakamani hapo.
Davina alikuwa kwenye mgogoro mzito na mwanaume huyo aliyezaa naye baada ya kumchukua mtoto, jambo lililomfanya mwanadada huyo aamue kumfuata ofisini na huko ndiko timbwili la Asha Ngedere lilikoanzia.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine