Saturday, December 3, 2011

PROFESA JAY KUJENGA STUDIO MJENGONI KWAKE



Siku chache baada ya kuhamia kwenye nyumba yake aliyojenga mbezi ya kimara dare s salaam, Hiphop Legend wa TANZANIA Profesa J, ameamplfy kwamba mpango unaofata ni kujenga studio ya muziki nyumbani kwake.
kutokana na kufatwa sana nyumbani kwake na wasanii wachanga wanaohitaji msaada wake, Prof amesema lengo ni kufaham vipaji vipya na kuwawezesha kupitia POFESA JAY FOUNDATION FOR TANZANIA COMMUNITY .
Kuhusu kuproduce nyimbo yeye mwenyewe, Prof amesema hayuko
vizuri kwenye swala la upigaji wa vyombo ila ataweka mawazo yake mengi katika record yoyote, atakachokifanya baada ya kujenga studio ni kutafuta producer mzuri kwa ajili ya kudili na hiyo kazi.

Bado haijajulikana ataianzisha lini rasmi hiyo wala itakamilika lini kwa sababu hata ujenzi bado haujaanza ila mpango uko mbioni.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine