Akiwa anatokea jijini Dar es salaam kuelekea mjini Morogoro akiwa anaendesha mwenyewe gari yake,Mbunge wa viti maalum kutoka Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi. Regia Mtema amefariki leo asubuhi majira ya saa tano huko Ruvu mkoani Pwani baada ya kupata ajali.Ajali hiyo imetokea wakati Bi. Regia akiwa kwenye harakati za kulipita gari lingine lililokuwa mbele yake na ghafla alipoteza mwelekeo
na kisha gari lake kupinduka,pia ndani ya gari hilo alikuwa na familia yake ikiwemo mama wa mbunge
huyo ambaye ni majeruhi na watu wengine watatu ambao wote ni majeruhi na wamelazwa kwenye hospitali ya Tumbi koani Pwani kwa matibabu.
Hili ndilo gari la mheshimiwa alilopata nalo ajali.
0 comments:
Post a Comment