KAMPUNI ya The Land ya China imetoa jezi seti 35 ambazo ni sawa na jezi 600 kwa timu ya Coastal Union na kuifanya timu hiyo kuweka rekodi ya kuwa na jezi nyingi zaidi nchini. Mkurugenzi wa kampuni hiyo ambayo inauza pikipiki aina ya Sound Motorcycle hapa nchini, Seleman Al-Khiyary amethibitisha kutoa jezi hizo ambazo zimetumiwa na Coastal Union katika mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar. Ni kweli tumetoa jezi 600 ambazo ni sawa na seti 35 zilizokamilika kwa Coastal Union tukiwa na lengo la kuisaidia timu hii kurudisha hadhi yake ya zamani,� alisema Al-Khiyary. Ofisa Habari wa Coastal Union, Edo Kumwembe alithibitisha kupokea kwa jezi hizo huku akisisitiza kwamba huo ni mwanzo wa kuirudisha Coastal katika anga za juu. |
0 comments:
Post a Comment