Monday, February 6, 2012

IVO MAPUNDA ALAMBA SH3.7 MILIONI ZA USAJILI

Ivo Mapunda
 











MTANZANIA aliyekuwa anaidakia Bandari FC, Ivo Mapunda ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki cha usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Kenya msimu huu.

Kulingana na orodha iliyotolewa na KPL katikati ya wiki, Mapunda aliyewahi kuwa kipa wa timu ya taifa ya Tanzania, amesajiliwa na klabu ya Gor Mahia FC kwa kiasi cha Sh200,000 za Kenya ambazo ni sawa na Sh3,711,590 za Tanzania.

Wanasoka wengine watatu waliosajiliwa kwa kiasi hicho ni Yusuf Juma kutoka Thika United kwenda Gor Mahia, Kevin Amwayi wa Western Stima na Wycliffe Ochomo wa Gor Mahia, waliosajiliwa na klabu ya Ulinzi Stars.

Hata hivyo, mchezaji aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa msimu huu ni Eric Masika kutoka Gor Mahia hadi kwa wapinzani wao wa jadi AFC Leopard. Mchezaji huyo amesajiliwa kwa kiasi cha Sh8,351,080.

AFC Leopards pia imemsajili Mganda, Abbas Kwalabye kutoka Chemelil Sugar kwa kiasi cha Sh7,052,020 kama ilivyokuwa kwa Allan Lwanga aliyekuwa akichezea klabu ya Hagl ya Vietnam.

Gor Mahia imemsajili mwanasoka wa Sony Sugar, Hugo Nzangu, ambaye ni mkimbizi kutoka Congo kwa Sh2,783,690 hali mkimbizi mwingine wa Congo, Patrick Kagogo aliyekuwa akichezea Sofapaka amesajiliwa na klabu bingwa ya Tusker FC.

Wanasoka wengi kutoka klabu mbili za Pwani, Congo United na Bandari wamesajiliwa na klabu za KPL kwa bei ya chini ya Sh92,789.7.

Wanasoka wawili wa Bandari, Andrew Murunga na Wycliffe Kasaya wamesajiliwa na Tusker na Gor Mahia mtawalia.

Wanasoka wa Congo waliosajiliwa kwa kiasi hicho cha Sh92,789.7ni pamoja na aliyekuwa nahodha na kiungo wa klabu hiyo, Ramadhan Athman Mbuggus aliyesajiliwa na Gor Mahia hali mkimbizi kutoka Nigeria, Morris Dukuly na Ben Wekes walilipiwa Sh371,159 kila mmoja na klabu za Thika United na Oserian mtawalia.

Amon Mwamburi na Hassan �Rio� Mohamed wote kutoka Congo United walisajiliwa na Ulinzi Stars na kwa Sh92,789.7 kila mmoja hali Nathan Munai akasajiliwa na Karuturi Sports kwa kiasi ambacho hakikutajwa.

Wachezaji wanne wa Congo United, Jude Kakan, Boniface Onyango, Mark Ongwae na Alex Nyamweno walijiunga na Nairobi City Stars kwa Sh92,789.7 kila mmoja

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine