Kocha wa Manchester City Roberto Mancini amekiri Carlos Tevez anaweza kucheza tena katika kikosi chake ikiwa atamshawishi kwamba yupo fit .
Japokuwa na imani kubwa iliyokuwa imetawala kwamba mshambuliaji huyo mwenye miak 27 angekuwa ameshaondoka City katika kipindi cha usajili, Tevez amebaki na City baada ya timu kama AC Milan, Inter Milan, na PSG kufaeli kumsaini kwa dili la kudumu.
Tevez kwa sasa bado yupo Argentina na kumekuwa hakuna uhakika wowote Carlitos atarejea lini England.
Japokuwa, Mancini ambaye siku za nyuma aliwahi kusema haifikiriki kwa Tevez kuvaa tena jezi ya Man City, lakini sasa muitaliano huyo amemtaja Carlitos katika majina ya wachezaji 25 watakaotumika katika premier league.
“Carlos sio chaguo kwa sasa lakini inawezekana huko mbeleni akarudi kucheza hapa,” alisema Mancini.
“Nina matumaini kwamba amekuwa akifanya mazoezi katika kipindi cha miezi 3 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment