Sunday, February 5, 2012

SIMBA YAGONGWA NA VILLA SQUAD VODACOM PREMIER LEAGUE

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam leo imekubali kipigo kutoka kwa Villa SQUAD katika mfulululizo wa ngwe ya lala salama ya Vodacom Premier League.
Katika mchezo huo uliofanyika jijini DSM katika uwanja wa taifa Villa ilifanikiwa kuondoka na pointi 3 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Villa ambao walimaliza mchezo huo wakiwa 10 dimbani walifunga goli lao katika dakika ya 40 likiwekwa kimiani na Nsa Job.
Katika hatua nyingine Coastal Union ya Tanga imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Moro United 1-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Chamazi – Dar es Salaam. Goli la Coastal lilitiwa kimiani na Rashid Yusuf katika kipindi cha pili.
Mashabiki wa Simba wakiwa wameduwaa uwanjani baada ya goli kufungwa.

Matokeo mengine ya VPL Ruvu shooting wametoka sare pacha na Polisi Dodoma.


0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine