Tuesday, February 7, 2012



TIMU ya Azam FC, jana ilifanikiwa kuishusha Yanga kutoka nafasi ya pili hadi  ya tatu baada ya kuichapa, JKT Oljoro, mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Azam imefanikiwa kufikisha pointi 32 na kukwea mpaka nafasi ya pili ikiipiku Yanga yenye pointi 31.
 Mshambuliaji wa kutegemewa wa Azam, John Bocco, alifunga bao la kwanza katika dakika ya 23 na kufikisha idadi ya mabao 11 na kuzidi kujichimbia kileleni mwa chati ya wafungaji bora akimpiku Kenneth Asamoah wa Yanga kwa tofauti ya mabao mawili.
Wafungaji wengine walioifungia Azam ni Mrisho Ngassa aliyefunga katika dakika ya 27 na lingine likifungwa kiungo mchezeshaji Abdi Kassim ‘Babi’ katika dakika ya 54.
Kwa matokeo hayo, Azam imebakiza pointi mbili kuikuta Simba kileleni baada ya mnyama kufungwa na Villa Squad juzi.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine