WASHINDI
wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC
watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu
kama Kombe la Kagame Julai, mwaka huu, Dar es Salaam, imeelezwa.
Kuingia
kwa Azam kwenye michuano hiyo, iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka
1974, kunamaanisha Tanzania Bara, wenyeji watawakilishwa na timu tatu,
nyingine zikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga na mabingwa wa
Ligi Kuu, Simba SC.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja
amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya michuano hiyo,
yanaendelea vizuri na tayari wadhamini wamekwishapatikana na
watatangazwa katika Mkutano maalum hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment