Saturday, May 26, 2012

Chelsea yawatosa Kalou, Bosingwa




















CHELSEA imefungua milango kwa nyota wake wawili Salomon Kalou na Jose Bosingwa kuondoka klabuni hapo wakati mikataba yao itapomalizika mwezi ujao.


 
Klabu hiyo leo inategemea kutangaza orodha ya wachezaji itakawaacha pamoja na mshambuliaji Didier Drogba.

Kalou, 26, alisajiliwa kutoka Feyenoord mwaka 2006 kwa gharama ya pauni 8m. Bosingwa, 29, alinunuliwa kwa pauni 16.2m kutoka Porto mwaka 2008.

Wawili hao kwa pamoja walianza kwenye kikosi cha kwanza kulichochukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga Bayern Munich kwa mikwaju ya penalti wiki iliyopita.

Bosingwa, ambaye amecheza mechi 127 kwa Chelsea, bado amebakiza mwaka moja kwenye maktaba wake wa sasa Stamford Bridge, lakini klabu hiyo haina mpango wa kuendelea naye.

Kalou mwenyewe amecheza zaidi ya mechi 250 na kufunga mabao 60 akiwa na jezi ya Chelsea.

Klabu kadhaa zimeshaonyesha nia ya kutaka kumsajili Kalou pamoja na  Liverpool, Arsenal na Tottenham, kama atashindwa kufikia mwafaka na Chelsea.

Inajulikana ni wazi mshambuliaji huyo anataka kubaki England, lakini sasa milango ipo wazi kwake kwenda  Italia, Hispania, Uholanzi au Uturuki.

Florent Malouda, Michael Essien na Paulo Ferreira wote wamebakiza mwaka moja kwenye mikataba yao ya sasa na wanaonekana wanaweza kuingia kwenye meza ya majadiliano msimu huu.

Frank Lampard pia amebakiza miezi 12 ya kubaki hapo, lakini anategemea kupata mkataba mpya.

Wakati huohuo; Chelsea imetoa pauni 32.4 milioni ili kupata saini ya kiungo wa Sao Paulo na Brazil, Lucas Moura.

Moura, 19, tayari amezivutia klabu nyingi za Ulaya kutokana na kiwango chake anachokionyesha kwa sasa katika klabu yake na timu ya taifa.

Kiungo huyo mshambuliaji tayari ameshacheza mechi 11 kwa timu ya taifa na rais wake Juvenico ameweka bayana kuwa nyota huyo ataondoka kwa dau kubwa tu.

Juvenico alidai kuwa Inter Milan na Real Madrid wameshaonyesha nia ya kutoa pauni20.2milioni kwa ajili ya kiungo huyo.

Lakini baada ya Chelsea kutangaza dau hilo kubwa, Juvenico anaamini mabingwa hao wapya wa Ulaya wanaweza kupata saini ya Moura.

"Tulikuwa hatutaki kupokea dau lolote, lakini Chelsea sasa wameonyesha kweli wanataka kumsajili Lucas," aliimbia tovuti www.fcinter1908.com.
                   
 

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine