TWIGA STARS YATUA SALAMA ETHIOPIA
Timu
ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Twiga Stars) imewasili sala
nchini Ethiopia jana tayari kwa mchezo wake dhidi ya wenyeji utakaopigwa
keshokutwa kwenye Uwanja
wa Addis Ababa wakati ile ya marudiano itachezwa Juni 16 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa
Ethiopia itakuwa imepeta tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.
Msafara
wa timu hiyo ambao kabla ya kuondoka ulikabidhiwa Bendera ya Taifa na
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
Twiga itacheza
na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya
mchujo kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake
(AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu Equatorial Guinea.
Wachezaji
walioondoka na kikosi hicho ni Amina Ally, Asha Rashid (nahodha), Ester
Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri,
Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma
Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia
Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.
Kwa
upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra
Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis (Meneja wa Timu), Mwanahamisi
Abdallah (Mtunza Vifaa) na Christina Luambano (Daktari wa Timu).
Twiga
Stars ambayo msafara wake unaongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira
wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itarejea
nyumbani Mei 28 mwaka huu saa 6 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
LIGI YA TAIFA KUANZA MEI 27
Ligi
ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa sasa itaanza Mei 27 mwaka
huu badala ya Mei 26 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali. Uamuzi
wa kusogeza mbele kwa siku kuanza kwa ligi hiyo uliofanywa na Kamati ya
Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana
jana (Mei 23 mwaka huu).
Timu
23 zitachuana katika kinyang’anyiro hicho kitakachofanyika katika vituo
vya Kigoma (Uwanja wa Lake Tanganyika), Musoma (Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume) na Mtwara (Uwanja wa Umoja) ambapo kinatarajia kumalizika Juni
13 mwaka huu.
Kituo
cha Kigoma kina timu za Aston Villa ya Singida, Bandari (Kagera), CDA
(Dodoma), JKT Kanembwa (Kigoma), Majimaji (Tabora), Mwadui (Shinyanga)
na Pamba (Mwanza).
Ashanti
United ya Ilala, Flamingo (Arusha), Forest (Kilimanjaro), Korogwe
United (Tanga), Nangwa VTC (Manyara), Polisi (Mara), Red Coast
(Kinondoni) na Tessema ya Temeke ziko kituo cha Musoma.
Kituo
cha Mtwara kina timu za Kurugenzi ya Iringa, Lindi SC (Lindi), Mighty
Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers (Morogoro), Mpanda Stars (Rukwa),
Ndanda (Mtwara), Super Star (Pwani) na Tenende (Mbeya).
CHANZO CHA HABARI: www.mamapipiro.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment