Mechi
ya kirafiki ya kimataifa kati ya Twiga Stars na Afrika Kusini (Banyana
Banyana) iliyofanyika Mei 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 8,012,000.
Mapato
hayo yametokana na washabiki 6,418 waliokata tiketi kushuhudia pambano
hilo kwa viingilio vya sh. 1,000, sh. 5,000 na sh. 1,000. Washabiki
6,057 walikata tiketi z ash. 1,000.
Asilimia
18 ya mapato ambayo ni sh. 1,222,169 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh.
1,560,000), waamuzi (sh. 650,000), usafi na ulinzi (sh. 1,000,000),
maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing
Construction (sh. 500,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa
upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 475,966,
asilimia 10 ya uwanja sh. 237,983, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) sh. 118,992 na asilimia 65 ya TFF (sh. 1,546,890).
0 comments:
Post a Comment