Makamu
wa Rais wa Kampuni ya Etisalat, Ahmed Mokhles akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampuni yao kudhamini shindano
la kusaka vipaji la Bongo Star Search, kulia kwake ni mkurugenzi wa
Benchmark Productions iyoandaa shindano hilo, Rita Poulsen.
Shindano la BSS mwaka huu litajulikana kama ‘Epiq Bongo Star Search’ ambapo mshindi atanyakua shilingi
milioni
50,pamoja na zawadi nyingine kutoka Zantel, sambamba na mkataba wa
kurekodi ili aweze kuendeleza kipaji chake baada ya shindano hilo. Aidha, mchakato wa mwaka huu utawahusisha washiriki kutoka mikoa nane
tofauti ikiwemo Zanzibar, Lindi, Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga, Dodoma na Dar es
Salaam ambapo mchakato utaanza mwezi Juni.
0 comments:
Post a Comment