Saturday, June 23, 2012

FLOYD MAYWEATHER NDIO MWANAMICHEZO ANAYEINGIZA MPUNGA MREFU KWASASA DUNIANI



Bondia wa Marekani Floyd Mayweather Jr. aka Money ameumaliza utemi wa miaka mingi wa mcheza gofu maarufu duniani Tiger Woods kama mwanamichezo anayeingiza fedha nyingi zaidi duniani na yeye kuishikilia nafasi hiyo sasa.
Bingwa huyo wa masumbwi ambaye kwa sasa yupo jela akitumikia kifungo cha siku 90, amemaliza ufalme wa miaka kumi wa Tiger kama mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwenye orodha mpya (2012) ya jarida la Forbes.
Mapambano aliyoshinda baada ya kuzichapa na Victor Ortiz pamoja na Miguel Cotto, yamemuingiza dola milioni 85.
Mpinzani wake Floyd, mfilipino Manny Pacquiao amekamata nafasi ya pili na kumsukuma Tiger nafasi ya tatu akiwa ameingiza dola milioni 62.
Tiger akiwa nafasi ya tatu aliingiza dola milioni 59.4.
Wanamichezo wengine waliomo kwenye list hiyo ni kama ifuatavyo:
4. LeBron James (NBA) – dola milioni 53.
5. Roger Federer (Tennis) – dola milioni 52.7.
6. Kobe Bryant (NBA) – dola milioni 52.3.
7. Phil Mickelson (Golf) – dola milioni 47.8.
8. David Beckham (Los Angeles Galaxy) – dola milioni 46.
9. Cristiano Ronaldo – dola milioni 42.5.
10. Peyton Manning (NFL) – dola milioni 42.4.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine