WANASAYANSI
mbalimbali wanaoendesha tafiti mbalimbali za kutafuta tiba na chanjo ya
Ukimwi, wameitangazia dunia kuwa hatua waliyofikia sasa wanauona
ugonjwa huo ‘siyo hatari tena’ kwa sababu wanazo silaha zote za kuweza
kukabiliana nao.
Ila
wakasema, kinachowakwamisha ni ukosefu wa fedha ambazo zinahitajika
katika kuendeleza tafiti na kuweka sera mpya za kukabili Virusi Vya
Ukimwi (VVU) duniani.
Hayo
yalibainika kwenye siku ya pili ya Mkutano wa 19 wa Kimataifa wa Ukimwi
unaofanyika mjini Washington DC, Marekani na unahudhuriwa na watu zaidi
22,000 miongoni mwao wakiwamo wataalamu wa afya, watunga sera na wadau
wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo toka karibu kila kona ya dunia.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo cha
Habari cha Mkutano huo na gazeti hili kufanikiwa kupata nakala yake,
ilieleza kwamba jopo la wanasayansi nguli duniani walikiri kuwa
wamefanyia VVU utafiti wa kutosha ndiyo maana wanatamba kuwa
wamefanikiwa katika kuvidhibiti.
“Kwa
sasa tunazo silaha zote za kisayansi kumalizia mbali gonjwa hili la
Ukimwi. Kilichobaki ni kutumia kikamilifu utaalamu huu katika fursa hii
tuliyo nayo,” alisema Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya
Mapambano dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira.
|
0 comments:
Post a Comment