Waziri wa dini wa Sudan Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim ni miongoni mwa watu 31 waliouwawa katika ajali ya ndege.
Shirika la habari la Sudan limesema
kuwa mawaziri wengine wawili na pia viongozi wa chama kinachotawala cha
Omar el-Bashir pia waliuwawa.
Ndege hiyo ya abiria ambayo pia ilikuwa imebeba wakuu kadhaa wa kijeshi ilianguka katika eneo la milima ya Nuba
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea eneo la Kordofan ya Kusini kwa sherehe za Eid al-Fitr ili kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mbali na waziri huyo wa maswala ya
kidini Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim wengine waliofariki katika ajali hiyo
ni mwenyekiti wa chama, Makki Ali Balayil,
waziri wa vijana na michezo, na Issa
Daifallah, waziri wa utalii na wanayma pori. Ndege hiyo ilianguka katika
eneo la Talodi huko Kordofan ya Kusini, ikiwa imetoka mji mkuu Khartoum
Mji huo wa Talodi, uko kilomita 50 kutoka mpaka wa Sudan Kusini.
Taarifa za runinga ya taifa zinasema
kuwa hali mbaya ya anga iliizuia ndege hiyo kutua na ilipojaribu mara ya
pili iligonga mlima.
Afisa mmoja wa shughuli za ndege
alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ya aina ya Antonov. Katika miaka ya hivi
karibuni kumekuwa na ajali kadhaa mbaya za ndege.
Maafisa wa Sudan wamekuwa wakilalamika kuwa imekuwa vigumu wao kupata vipuri kwa sababu ya vikwazo vya Marekani.
0 comments:
Post a Comment