Mwezi Agosti
Wigan Athletic
Wigan Athletic
Klabu ya
Wigan Athletic imekamilisha usajili kwa kutiliana saini na mchezaji Ivan
Ramis kutoka klabu ya Mallorca kwa kitita cha takriban Euro milioni 6.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 alitarajiwa kujiunga na West Ham baada
ya tangazo la Mallorca kudai kua wamekubaliana na West Ham juu ya beki
huyo lakini yeye binafsi akafikia makubaliano na Wigan kwa mkataba wa
miaka mitatu. Ramis ameichezea Mallorca mara 103 katika La Liga ya
Uhispania tangu mwaka 2004. Huyu ni mchezaji wa pili kusajiliwa na kocha
Roberto Martinez baada ya Fraser Fyvie kutoka Aberdeen.
Everton:Malipo ya Pienaar yaafikiwa
Klabu
ya Everton imeafikiana malipo kwa mcheza kiungo wa klabu ya Tottenham
Hotspur Steven Pienaar. Klabu hiyo inayochezea kwenye uwanja wa Goodison
Park imekua na hamu kumsajili mchezaji wake hapo zamani ikiwa alihamia
Tottenham kutoka Everton mwezi Januari mwaka 2011. Pienaar alirudi
Everton kwa mkopo mnamo mwezi Januari mwaka 2012 baada ya kushindwa
kufikia viwango vya Spurs. Lakini aliporejea Everton alishiriki mechi 14
akifunga mabao 4 na kuibua kipaji kilichomfanya kuwa nyota katika mwaka
2007.
Unior Hoilet ahamia QPR
QPR
imemsajili mcheza winga ya kushoto Junior Hoilett kwa mkataba wa miaka
minne kutoka klabu ya Blackburn Rovers. Huyu ni mchezaji wa saba
kusajiliwa na kocha
Mark Hughes, akifuata wachezaji Rob Green, Ryan Nelsen, Fabio Da Silva,
Ji-Sung Park, Samba Diakite na Andy Johnson. Kijana huyo kutoka Canada
alikua huru bila klabu yoyote baada ya kukataa kutia saini mkataba mpya
na Blackburn Rovers, kufuatia klabu hio kushuka daraja hadi mashindano
ya Championship.
Vlaar ajiunga na Aston VillaAston
Villa imekamilisha usajili wa beki wa klabu ya Feyenoord Ron Vlaar kwa
mkataba wa miaka mitatu akisubiri kukamilisha utaratibu wa afya wiki
hii.
Vlaar alikua kwenye kikosi cha Uholanzi wakati wa
mashindano ya Euro 2012, na alikua huko Villa Park hivi karibuni kwa
majadiliano na kocha mpya Paul Lambert. Beki huyo anatazamiwa kupitia
utaratibu wa afya jumatatu kukamilisha usajili wake kutoka klabu ya
Feyernoord.
Chelsea yakamilisha usajili wa Oscar.
Klabu
ya Chelsea imehitimisha usajili wa mcheza kiungo kutoka Brazil Oscar
aliyekua akichezea klabu ya Internacional kwa kitita cha Euro milioni
€32m. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 yuko kwenye kikosi cha Taifa
cha Brazil kinachoshiriki mashindano ya Olimpiki.
Oscar alianza
kucheza soka akiwa katika klabu ya Sao Paulo kabla ya kuhamia
Internacional mnamo mwaka 2010. Katika kipindi hicho alifunga mabao 11
katika mechi 36 za Ligi.
Chelsea vilevile imemsajili ndugu yake nyota Hazard kutoka Ufaransa aliyesajiliwa na klabu hio mapema Thorgan Hazard.
Tottenham.
Mpango wa Modric kujiunga na Real Madrid bado una ati ati
Meneja wa Tottenham Andre Villas-Boas ameonya vilabu vinavyomtaka kiungo wake Luka Modric kua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 haondoki hadi anayemtaka atimize kitita cha pauni milioni 35 ilichodai Spurs. Kwa kipindi cha mwaka mzima majaliwa ya kiungo huyo yamekua gumzo ambapo Real Madrid imeongoza kwa vilabu vinavyomtaka ajiunge navyo. Lakini Real Madrid imeshikilia msimamo wa kua hawazidishi pauni milioni 27.
Mpango wa Modric kujiunga na Real Madrid bado una ati ati
Meneja wa Tottenham Andre Villas-Boas ameonya vilabu vinavyomtaka kiungo wake Luka Modric kua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 haondoki hadi anayemtaka atimize kitita cha pauni milioni 35 ilichodai Spurs. Kwa kipindi cha mwaka mzima majaliwa ya kiungo huyo yamekua gumzo ambapo Real Madrid imeongoza kwa vilabu vinavyomtaka ajiunge navyo. Lakini Real Madrid imeshikilia msimamo wa kua hawazidishi pauni milioni 27.
0 comments:
Post a Comment