Wednesday, August 8, 2012

BRAZIL NA TANZANIA ZAENDELEA KUSHUKA VIWANGO VYA UBORA WA SOKA DUNIANI


Timu ya Taifa ya Spain imeendelea kukalia kiti cha uongozi wa ubora wa soka kwa mujibu wa viwango vya FIFA. Mabingwa hawa dunia na ulaya wameshikilia uongozi huo wakiwa na pointi 1605, nafasi ya pili imekamatwa na Ujerumani, nafasi ya tatu imechukuliwa na England wakiendelea kupanda ubora kwenye rank hizo za FIFA bada ya mwezi uliopita kushika nafasi ya nne.

Brazil mabingwa wa mara tano wa dunia wameendelea kuweka rekodi, baada ya kushika nafasi ya 13 chini zaidi.

Ivory coast ndio pekee ya kiafrika kuwemo ndani ya 20 bora, wakishika nafasi ya 16. Timu ya taifa ya Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 127 mpaka 128.







            
























0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine