KILA WIKI SIKU YA JUMATANO TUTAKULETEA JINSI YA KUPIKA VYAKULA MBALIMBALI.Leo tunakuletea Mapishi ya Pilau ya nyama ya ng'ombe na kachumbari.
Mahitaji
- Mchele (rice vikombe 3)
- Nyama ya ng'ombe (beef 1/2 kilo)
- Viazi mbatata (potato 3)
- Vitunguu maji (onions 3)
- Kitunguu swaum (garlic cloves 4)
- Tangawizi iliyosagwa (ginger kiasi)
- Hiliki nzima (cardamon 4)
- Karafuu (clove 4)
- Pilipili mtama (blackpepper 4)
- Amdalasini (cirnamon stick 1)
- Binzari nyembamba nzima(cumin seeds 1/2 ya kijiko cha chai)
- Binzari nyembamba ya kusaga (ground cumin 1 kijiko cha chai)
- Chumvi (salt)
- Mafuta (vegetable oil)
- Nyanya (fresh tomato 3)
- Limao (lemon 1)
- Pilipili (chilli 1)
- Hoho (green pepper)
Matayarisho
Chemsha nyama na chumvi na nusu
ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya
pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na
kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya
moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta
kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi
ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown
pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri
kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni
Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama
na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko
uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na
viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri
kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia
kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke
kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive.
Baada ya hapo andaa kachumbali kwa kukatakata
vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali
wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya,
Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na
vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote
pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.
0 comments:
Post a Comment