Watu wenye silaha wamewafyatulia risasi waumini waliokuwa kwenye ibada kanisani jumanne huko kusini mwa Nigeria na kuwauwa watu wasiopungua 19 na kuwajeruhi kadhaa wengine.
Maafisa wa serikali ya Nigeria wanasema idadi ya watu wasiojulikana
waliokuwa na silaha walilishambulia kanisa la Deeper Life huko Okene
katika jimbo la Kogi. Maafisa wa usalama wanawatafuta washambuliaji
lakini hawajafanikiwa kumkamata mtu yeyote. Hakuna mtu yeyote anayedai
kuhusika na shambulizi hilo.
Kundi la ki-islam lenye msimamo mkali la Boko Haram limekuwa
likifanya mashambulizi kwenye makanisa kadhaa huko kaskazini na kati
kati ya Nigeria katika kipindi cha mwaka uliopita lakini Okene ipo
kusini zaidi ya eneo linalolengwa na kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment