Mahitaji
- Mchele (rice 1/2 kilo)
- Maharage yaliyochemshwa (boiled red kidney beans 1 kikombe cha chai)
- Samaki waliokaangwa ( 2 fried fish)
- Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 ya tin)
- Vitunguu vilivyokatwa (onion 2)
- Kitunguu swaum (garlic 3 cloves)
- Tangawizi (ginger kiasi)
- Limao (lemon 1/2)
- Chumvi (salt)
- Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
- Mafuta (vegetable oil)
- Spinach
- Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)
Matayarisho
Saga
nyanya, kitunguu, tangawizi na kitunguu swaum pamoja. Tia kwenye sufuria na
upike mpaka maji yakauke kisha tia curry powder, mafuta na chumvi na upike tena
mpaka mchanganyiko uive kisha tia samaki na limao na maji kiasi na uache
uchemke kiasi. Na hapo mchizi utakuwa tayari.
Osha na
uzikate spinach kisha kaanga kitunguu na mafuta kiasi (hakikisha visiwe vya
brown kisha tia spinach na chumvi. zipike kwa muda wa dakika 3-4 na hapo
zitakuwa tayari zimeshaiva.
Wali:
Chemsha maji kiasi kisha tia, chumvi, pilipili nzima(isikatwe) mafuta na tui la
nazi. Baada ya hapo koroga na utie mchele na maharage na ufunike uache uchemke
mpaka maji yakauke. Kisha geuza na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya
hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuseviwa.
0 comments:
Post a Comment