Wednesday, September 5, 2012

McCarthy kikosini Mechi ya kirafiki Africa kusini na Brazili

 
BenniMcCarthy, aliyekuwa akidaiwa kuwa kutokidhi viwango kiafya na kumfanya kushindwa kucheza Fainali za Kombe la dunia, katika hali ya kushtukiza, ameitwa na Timu yake ya taifa ya Afrika Kusini kwa ajili ya kujiunga na wenzake kucheza Mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil.
Hii ni mechi ya kwanza ya kimataifa kwa McCarthy kwa zaidi ya miaka miwili kwa Mshambuliaji wa zamani wa Blackburn Rovers na West Ham, aliyekosa kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 katika Ardhi yake, baada ya timu kumtema kwa kilichodiwa kuwa hakuwa imara kiafya.
Baada ya kucheza kwa zaidi ya muongo mmoja Barani Ulaya, ikiwemo ushindi wa Kombe la ligi ya mabingwa ambapo aliichezea porto chini ya Jose Morinho mwaka 2004.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alirejea nyumbanu Msimu uliopita na kufunga mara 12 na kushinda ligi ya nyumbani akicheza na timu mabingwa katika Ligi hiyo, Orlando Pirates

CHANZO CHA HABARI: www.kwetubongo.com

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine