Saturday, September 22, 2012

SIMBA NA YANGA KUCHEZA USIKU TAIFA OKTOBA 3 LIVE SUPER SPORT


Yanga SC
MECHI ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayopigwa Oktoba 3, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachezwa kuanzia Saa 1:00 usiku na kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha SuperSport.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema leo kwamba hiyo itakuwa moja kati ya mechi tano za Ligi Kuu zilizobatizwa jina Super Weekend katika mzunguko wa kwanza, ambazo zote zitaonyeshwa moja kwa moja na SuperSport, zikianza kati ya saa 1:30 jioni na saa 1:00 usiku.
Simba SC
Mechi nyingine ni za Septemba 28 mwaka huu kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku, Simba na Tanzania Prisons Septemba 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, Yanga na African Lyon Septemba 30, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 na Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar Oktoba 1, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10:30 jioni.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine