Mahitaji
Kambale 2
Nazi kopo 1
Nyanya kopo
1
Vitunguu 2
Curry
powder 1 kijiko cha chai
Turmaric
1/2 kijiko cha chai
Binzari
nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai
Swaum/
tangawizi 1 kijiko cha chakula
Giligilani
kiasi
Limao 1/2
Chumvi
Olive oil
Matayarisho
Loweka
samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga
pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike
mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta
kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi,
samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi
litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo
ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa.
Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali
mlaiiini au na wali pia.
0 comments:
Post a Comment