Mahitaji
- Viazi (potato 1/2 kilo)
- Samaki (fish 2)
- Asparagus 8
- Kitunguu kilichokatwa (chopped onion 1)
- Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic 4 cloves)
- Tangawizi iliyosagwa kiasi (ginger paste)
- Limao (lemon 1)
- Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander)
- Curry powder (kijiko 1 cha chai)
- Chumvi (salt)
- Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Safisha
samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa
muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan
kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji
na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke
samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani
iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya
vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika
vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada
ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama
vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza
mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na
giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya
hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza
zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko
katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike
kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari
kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.
0 comments:
Post a Comment