ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Barnabas
Mtokambali, amekemea vitendo vya baadhi ya wanaume wanaovaa suruali
chini ya makalio, akisema wanaofanya hivyo ni sawa na mashoga.
Alisema mwanamume kuvalia suruali chini ya makalio ni sawa na kujitangazia biashara ya ushoga ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Mtokambali
alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua Chuo cha Ualimu cha Mount Sinai
kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema
kama ilivyokuwa kwa machangudoa ambao huvaa nusu uchi kuonesha kuwa
wapo katika biashara, ndivyo hivyo kwa mashoga nao wanavaa ili
kujitambulisha.
Kutokana
na kukithiri kwa vitendo hivyo, aliwaasa wanafunzi wa chuo hicho kuvaa
kwa kuzingatia maadili ili wawe walimu bora kwa taifa na mfano wa
kuigwa.
Makamu
Mkuu wa chuo hicho, Alexander Chuwa, alisema licha ya chuo hicho kutoa
mafunzo ya ualimu, pia kinatoa mafunzo ya elimu ya biashara na malengo
ya baadaye ni kuwa chuo kikuu.
chanzo:daima
0 comments:
Post a Comment