Wednesday, February 27, 2013

YANGA 1 - 0 KAGERA SUGAR


Dk 90+5 FULL TIME. YANGA 1-0 KAGERA.

Dk 89 Mkina wa Kagera anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Yanga.


Dk 85 Ngwai wa Kagera anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mbuyu Twite.


Dk 79 Mwamuzi Mberwa anawapa kadi za njano wachezaji wa akiba wa Yanga, Nizar Khalfan na David Luhende baada ya kuacha kufanya mazoezi na kusimama wakitazama mpira wakiwa jirani na benchi lao.


Dk 73 Cannavaro anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Paul Ngwai wa Kagera.


Dk 73 Chuji anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Shija Mkina wa Kagera.

Dk 71 Kagera imefanya mabadiliko, ametoka Enyinna, ameingia Themi Felix.

Young Africans inafanya mabadiliko wanaingia Jerson Tegete na Hamis Kiiza kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi


Dk 70 Goooooooal Haruna Niyonzima anaipatia Yanga bao la kwanza


Dk 63 Themi Felix wa Kagera anapasha misuli moto.


Dk 62 Kagera imefanya mabadiliko, ametoka Mrope, ameingia Paul Ngwai.


Dk 60 Said Bahanunzi wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano.


Dk 56 Wachezaji wa akiba wa Yanga, Jerry Tegete na Hamis Kiiza wanapasha misuli moto.


Dk 48 Frank Domayo wa Yanga anapiga shuti kali limalogonga mwamba wa lango la Kagera na kurudi uwanjani baada ya kupokea pasi ya Niyonzima.


Dk 46 Chuji anamchezea faulo Nade wa Kagera. Yanga 0-0 Kagera.


Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!


Dk 45+3 HALF TIME! YANGA 0-0 KAGERA.


Dk 45+3 Kavumbagu wa Yanga anapiga penalti lakini anakosa baada ya mpira alioupiga kupaa juu ya lango la Kagera. Yanga 0-0 Kagera.


Dk 45+2 Kagera wanakubali penalti ipigwe lakini kipa wao Kalyesubula anaonyeshwa kadi ya njano kwa kitendo cha kugomea penalti hiyo kwa kwenda katika benchi la timu yake.


Dk 45 PENAAALTY...! Yanga inapata penalti baada ya mshambuliaji wake Didier Kavumbagu kuangushwa katika eneo la hatari na kipa wa Kagera, Kalyesubula. Kagera wanagomea penalti.


Dk 44 Oscar Joshua wa Yanga anapiga shuti kali kuelekea lango la Kagera na mpira unatoka nje.


Dk 43 Safu ya kiungo ya Yanga inapwaya na kupoteza pasi nyingi huku Kagera wakionekana kuzinduka na kucheza soka safi.


Dk 41 Haruna Niyonzima wa Yanga anamvuta jezi Muganyizi Martin na mwamuzi anaamuru ipigwe faulo kuelekea lango la Yanga.


Dk 39 Julius Mrope wa Kagera anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Athuman Idd Chuji.


Dk 32 George Kavila wa Kagera anapiga faulo inayotoka juu ya lango la Yanga.


Dk 31 Beki Oscar Joshua wa Yanga anamchezea vibaya Juma Nade wa Kagera na mwamuzi anaamuru ipigwe faulo kuelekea lango la Yanga.


Dk 29 Benjamin Asukile wa Kagera anamwangusha Msuva nje kidogo ya eneo la hatari la Kagera na mwamuzi Simon Mberwa wa Pwani anaamuru ipigwe faulo kuelekea lango la Kagera.


Dk 27 Kagera wamebadilika sasa wanatawala kiungo na kulifikia lango la Yanga mara kadhaa.


Dk 27 Kagera wamebadilika sasa wanatawala kiungo na kulifikia lango la Yanga mara kadhaa.


Dk 23 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' anaumia baada ya kugongana na mshambuliaji wa Kagera Darlington Enyinna. Yanga 0-0 Kagera.


Dk 20 Mpira unasimama kwa muda kipa wa Kagera, Kalyesubula anarekebisha viatu vyake.


Dk 15 Kagera wanacheza kwa kuinda zaidi lango lao.


Dk 13 Msuva wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa Kagera lakini kipa Hannington Kalyesubula anaudaka mpira.


Dk 10 Yanga inacheza zaidi katika eneo la Kagera.


Dk 5 Yanga inapata kona baada ya Maregesi Mwangwa wa Kagera kuutoa nje mpira. Yanga 0-0 Kagera.


Dk 2 Didier Kavumbagu wa Yanga anakosa baada ya mpira wa kichwa alioupiga kugonga mwamba wa lango la Kagera.


Dk 1 Muganyizi Martin wa Kagera Sugar anamchezea vibaya Simon Msuva wa Yanga.


Young Africans line-up to face Kagera Sugar today:
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo 'Chumvi'
9.Said Bahanuzi
10.Didier Kavumbagu
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Nizar Khalfani
6.Hamis Kiiza
7.Jerson Tegete


KAGERA SUGAR LINE UP: Hannington Kalyesubula, Benjamin Asukile, Muganyizi Martin, Malegesi Mwangwa, Amandus Nesta (C), George Kavila, Julius Mrope, Juma Nade, Darlington Enyinna, Shija Mkina, Daudi Jumanne.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine