Tatizo jingine linaloathiri tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa wanaume wa umri mbalimbali duniani. Aidha ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wa umri miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwasasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25.
Nani yupo katika hatari ya kupata saratani ya tezi dume?
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na:
Wanaume wenye asili ya Afrika (weusi) ikilinganishwa na wazungu
Wanaume kuanzia miaka 60 na kuendelea
Wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
Wanaume wanaokunywa pombe kupindukia
Wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali
Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
Wachimbaji wa madini hususani aina ya cadmium
Walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama
Pamoja na kwamba, tatizo la kukua na kuongezeka kwa tezi dume yaani BPH hutokea kwa wanaume wengi, hali hiyo haiongezi uwezekano/hatari ya kupata saratani ya tezi dume.
Dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?
Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na
Kupata shida unapoanza kukojoa
Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
Kutoa mkojo uliochanganyika na damu
Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu za jirani ya mwili, mgonjwa anaweza kuwa na
Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
Aidha, mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
Saratani ya tezi dume inatibika?
Ndiyo! Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika.
Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi, wakati kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri kumfuatilia mgonjwa kwa ukaribu bila kumfanyia upasuaji au bila kumpatia tiba ya mionzi.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).
BIDHAA ZINAZOTIBU SARATANI YA TEZI DUME: CHILATED ZINC,TRE-EN-EN,MASQULINE,OMEGA 3 SALMON OIL PLUS.
Friday, March 29, 2013
Saratani ya Tezi Dume.
3/29/2013 09:18:00 AM
Unknown
No comments
0 comments:
Post a Comment