Utangulizi: chapati za maji ni kitafunwa au chakula kinachopendwa na na wengi. chakula hiki hupendwa zaidi na watu kwa sababu ni rahisi kutayarisha
Mahitaji
- Ngano 1/2 kilo
- mayai 3
- mafuta au samli 1/4 kikombe
- kitunguu kikubwa kilichosagwa !
- Thomu punje 4
- Chumvi 1/2kijiko
Namna ya kupika
- Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.
- Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito san a wala si mwepesi sana.
- Ongeza mayai na chunmvi endelea kukoroga .
- Ongeza kitunguu thomu na kitunguu maji .
- Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.
- Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekundetano hadikumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.
- Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.
- Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa.
- Fanya hivyo kwa chapati zote.
0 comments:
Post a Comment