Friday, May 3, 2013

UMEISIKIA HII: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YAFUTWA, MITIHANI KUSAHIHISHWA UPYA

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, akiwa bungeni mjini Dodoma.

HABARI zilizotoka bungeni mjini Dodoma muda huu ni  kwamba matokeo yote ya  kidato  cha  nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya haraka iwezekanavyo.
Taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne kwa mwaka jana imesomwa  leo bungeni  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Waziri Lukuvi amesema sababu zilizosababisha wanafunzi  hao kufeli ni pamoja na upungufu wa waalimu, mazingira magumu ya kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa  na  utaratibu  mbovu  wa  Baraza  la  Mitihani Tanzania (NECTA) uliotumika  bila  kuwashirikisha  wadau mbalimbali  wa  elimu.
Kutokana na sababu hizo, matokeo yote ya kidato cha nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine