KWA mara nyingine Arsenal inataka kumrejesha Nahodha wake wa zamani,Cesc Fabregas majira ha ya joto.
Kwa sasa kiungo huyo wa zamani wa The
Gunners yupo mapumzikoni baada ya kumaliza kuichezea Hispania kwenye
Kombe la Mabara na mustakabali wake Barcelona haueleweki kutokana na
msimu mbaya uliopita.
Taarifa nchini Hispania zimeendelea
kusema atabaki Nou Camp, lakini shaka inaletwa na namna atakavyoingia
kwenye mipango ya kocha Tito Vilanova baada ya msimu uliopita kutemwa
katika mechi zote kubwa.
Hana furaha? Mambo hayajaenda kama yaliyopangwa kwa Cesc Fabregas Barcelona
Dili la kumsajili tena Fabregas
halitakuwa na utata, kwa sababu wakati Arsenal inamuuza mchezaji huyo
Hispania kwa Pauni Milioni 25, ilipewa nafasi ya kwanza ya kumsajili
ikimhitaji.
Ikiwa Barca itaamua kumuuza Fabregas, The Gunners watapewa nafasi ya kwanza ya kumsajili kwa Pauni Milioni 25.
Wakati huo huo: The Gunners imefufua
mpango wa kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams kufuatia Thomas
Vermaelen kurejea kwenye maumivu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales ni
mtu anayetakiwa mno na Arsene Wenger majira haya joto, lakini Arsenal
haijafika bei ya dau la Pauni Milioni 10 linalotakiwa kwa ajili ya beki
huyo.
Nahodha Vermaelen anaweza akakosa
maandalizi ya mwanzoni mwa msimu kutokana na kuumia tena, na ataiacha
Gunners na mabeki wawili tu walio fiti; Laurent Koscielny na Per
Mertesacker.
Majeruhi kampa ulaji? Kuumia kwa Thomas Vermaelen kumeifanya Gunners ifufue mpango wa kumsajili Ashley Williams
0 comments:
Post a Comment