Thursday, August 15, 2013

YAFAHAMU MAGONJWA YA TABIA


Kuna magonjwa mengi yanayowatesa ma elfu ya watanzania na watu wengi wanashindwa kujua suluhisho la magonjwahayo lipo na mpaka wengine wakihusisha na imani za kushirikina.

Miongoni mwa magonjwa hayo ni upungufu wa nguvu za kiume na kike, vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye kuta za njia ya mfumo wa mmengenyo wa chakula, mgandamizo wa juu wa damu, moyo kutanuka, kisukari (kongosho kushindwa kufanya kazi vizuri).

Chanzo cha vidonda vya tumbo

Kuzalishwa kwa wingi kwa hydrochloric acid na hivyo acid hii kumengenya kuta za tumbo, lakini pia wasiwasi ikiwa mtu ana msongo wa mawazo itaathiri hamu ya kula na hivyo enzymes hazitakuwa na chakula cha kumengenya na badala yake itamengenya kuta za tumbo. 

Sababu nyingine inayosababisha vidonda vya tumbo ni kusahambuliwa kwa bacteria waitwao helicbacter pylori ambao wakiingia mwilini hushambuia kuta za tumbo na kuondoa nozi inayoziba juu na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.

Vyanzo vingine ni unywaji wa vinywaji vyenye caffeine, utumiaji wa dawa zenye sulfa kwa wingi kama asprin , ibuprofen, na nyinginezo, unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara n.k

Kwa kawaida kuna aina mbili za vidonda vya tumbo: aina ya kwanza ni vidonda vile ambavyo dalili zake kuu ni kuhisi maumivu hasa baada ya kula chakula. Aina ya pili ni vidonda vile vilivyoko kwenye utumbo mwembamba na dalili zake ni kuhisi maumivu hasa kabla ya kula.

Moyo kutanuka
Ugonjwa huu unafanya moyo kuwa dhaifu na kushindwa kusukuma damu vizuri kuelekea sehemu mbalimbali za mwili.


Sababu:

Misuri ya moyo kutanuka kutokana na kushambuliwa na sumu zilizoko mwilini, sumu hizo hushambulia seli zinazounda misuli ya moyo na hivyo kuifanya iwe dhaifu na kushindwa kusukuma damu mwili. Sababu nyingine ni Unywaji wa pombe, magonjwa ya tezi, shinikizo la juu la damu na sababu nyinginezo

Figo
Figo kazi yake kubwa na muhimu mwilini ni kuchuja taka zilizoko kwenye damu na kuchukua baadhi ya vitu vinavyohitajika mwilini na kurudisha kwenye mzunguko wa damu. Figo huchuja lita 180 kwa siku lakini ni lita 1.5 hadi 2 ndio hutolewa kama mkojo kwa siku kwa mtu mzima asiye na tatizo la kiafya.
Wakati mwingine figo hushindwa kufanya kazi zake kwa muda Fulani lakini hutibika. Dalili za figo kushindwa kufanya kazi vizuri ni kupungua kwa kiwango cha mkojo na kufikia chini ya 400ml kwa mtu mzima na chini ya 0.5ml kwa watoto. Mara nyingi ugonjwa huu huanza taratibuna huonyesha dalili chache, lakini baada ya muda tatizo huwa sugu na kuleta madhara makubwa. Figo inaposhindwa kuondoa maji mwilini inasababisha miguu, mikono, uso kuvimba, kushindwa kupumua vizuri na maji kujaa kwenye mapafu, kupoteza hamu ya kula, kushindwa kupata usingizi na ngozi kuwa nyeusi.
Mgandamizo wa juu wa damu
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa ya alteries na hivyo kuufanya moyo ufanye kazi zaidi ili uweze kusukuma damu
Kwa kawaida msukumo wa damu hutegemea wakati misuli ya maumivu ya kichwa hasa sehemu ya nyuma ya kichwa kupoteza uwezo wa macho kuona na kupoteza fahamu. Matumizi ya vyakula vyenye mafuta kwa wingi husababisha misuli ya moyo kulegea na kushinwa kufanya kazi inavyotakiwa. 


Magonjwa haya hutibika mara nyingi endapo mtu atazingatia sana jinsi anavyokula na kutumia dawa zinazotengenezwa na miti shamba, kama vile mizizi, mimema, viumbe wa baharini, (miti shamba). Watu wengi washatibiwa magonjwa haya kwa kupitia miti shamba na wengi wanaona matokeo yake mara waanzapo tiba mbadala. 

Mwili unahitaji virutubisho mbali mbali ili kuweza kupambana na magonjwa haya yanayosababishwa na tabia. Ni kweli kwamba kukwepa magonjwa haya ni vigumu sana kwasababu ya maisha tunayoishi na mazingira tuliopo sasa hivi. 

Teknolojia inavyozidi kukua kwa kasi ndivyo na mlipuko huu wa magonjwa unavyosidi kuongezeka na wengi wetu hukata tama baada ya kugundua una ugonjwa fulani lakini si kweli kwamba hautibiki bali ni utayari wa wewe kutibiwa. tutembelea "NewLife-Afya" ili uweze kujua suluhisho la tatizo lako, upe mwili virutubisho vinavyotakiwa ili mwili uweze kupambana na matatizo haya.

Wengi wetu tumekuwa hatufanyi mazoezi na kula ilimradi nimeshiba bila kuzingatia je mwili unapata mahitaji yake muhimu? Je kila siku wala vyakula visivyo na virutubisho vya wili je huo mwili hata ni nini usichakae? 

Gari ni chombo chenye spare party ambacho kikiharibia unauwezo wa kwenda dukani na kukipata na kuja kureplace lakini gari hilo hilo tunalipeleka service ili liweze kudumu kwa muda mrefu lisife mapema je mwili wako basi ni nini hata usiujali kama ujalivyo gari lako je huoni kuna sababu ya kula na kufanya kazoezi kwa wingi? 

Je huoni kunasababu ya kupima mara kwa mara na kuondoa sumu ziingiazo mwilini? Je huoni kunasababu ya kufuata mfumo mzuri wa kula ili kulinda afya yako?

Wataalamu wa masuala ya afya wanasema tule kulingana na jedwali linavyotuonyesha hapo chini, lakini kutokana na hali halisi ya maisha mazingira tunayoishi na kufanyia kazi na kipato nacho kinachangia sana wengi wetu tumeligeuza jedwali hili kuwa juu chini na chini juu yaani tunakula vyakula vya mafuta kwa sana, protini kwa wingi, matuna na mboga za majani ndio kidogo hata wakati mwingine hazipo na zikiwepo tumeziivisha kupita kiasi na kwenye nafaka ndio tunaongoza kwa ukoboaji. 

Je mwili wako utapambana vipi na magonjwa haya ya tabia? 

Je huoni kwamba unahitaji kweli kuuservice mwili wako kwa kiwango kikubwa? 

Je huoni kwamba mwili wako uko kwenye hatari kubwa sana ya mwili wako kushambuliwa na magonjwa? 

Tuone NewLife-Afya"  au PIGA SIMU +255752133700/+255713354389 kwa ushauri zaidi na suluhisho la afya yako.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine