Friday, September 6, 2013

UJUE UGONJWA WA PRESHA NA JINSI YA KUTATUA TATIZO:


Hii ni hali ambayo moyo husukuma damu kwa hali ambayo si yakawaida,presha(shinikizo la damu) husaidia ktk msukumo wa damu,lkn presha ikiwa kubwa kubwa inaweza kuleta madhara ya kiafya na huweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.Watu wazima zaidi ya umri wa miaka 18 presha ya dystole inatakiwa kuwa kipimo cha juu cha 120 mm Hg na presha ya diastole ambacho ni kipimo cha chini kabisa inatakiwa kuwa 80mm Hg,presha ya dystole ni kipimo ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu ktk mishipa ya damu wakati moyo unadunda.Presha ya diastole ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu ktk mishipa ya damu wakati moyo umepumzika au kati ya mapigo ya moyo.
Presha hupimwa ktk milimita za mercury,hapa ndipo tunasema presha inatakiwa kuwa 120/80 mm Hg


Ugonjwa huu anaweza kuupata mtu yeyote mkubwa au mtoto kulingana na maisha tunayoishi,Presha huathiri vitu vingi mfano Idadi ya maji mwilini,idadi ya chumvi,homoni mwilini,hali ya joto au hali ya baridi,hali ya hisia na hali ya mafigo,mfumo wa neva na mishipa ya damu.
Kama presha itakuwa juu na kuachwa kutodhibitiwa moyo na mishipa haitafanya kazi vizuri kama ipasavyo.Kwasababu neva na seli za mwili tayari zinakuwa zimeshaathiriwa na presha hapo ndipo mtu akitumia dawa zenye kemikali inakuwa ngumu sana kupona kabisa tatizo hilo.
Lakini usijali sasa utapona na utarudi kama kawaida kwa kufuata kile nitakachokuelekeza.
Kuna aina mbili za presha
1. Presha ya asili ambayo yenyewe amabayo chanzo chake hakifahamiki ,lkn tatizo la kigenetics na kimazingira kama,chakula,mazoezi zinanafasi kubwa ktk ugonjwa huu.
2. Presha inayosababishwa na tatizo kwenye mwili Mfano:Kupungua unene wa mishipa flani ya damu,Matatizo ya tezi,Matatizo ya figo,matumizi ya dawa ,madawa ya kulevya au kemikali,matumizi ya madawa ya kuzuia mimba


Hali zinazosababisha Presha

Hali ya unene wa kupindukia

Ulaji mwingi wa chumvi au sodium

Hali ya uvivu

Uvutaji wa sigara

Mazingira ya mifadhaiko ya hali ya juu

Ulaji wa vyakula visivyo vya afya

Historia ya kifamilia ya kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu

Jinsi Ya Kuzuia Ugonjwa Wa Presha

Acha uvutaji wa sigara

Pungua uzito kama ni mnene

Ongeza mazoezi ya viungo ili kuimarisha hali ya afya ya moyo

Punguza sodium iwe chini ya gramu 2.4 za sodium au chini ya gram 6 za chumvi kwa siku (chumvi kijiko kidogo kimoja na robo)

Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na kolestero

Punguza unywaji wa pombe ( tumia kinywaji kimoja au viwili kwa siku)

Ulaji wa kiwango kinachotakiwa cha kalsiumu, potasiamu, magnesiamu,

Dhibiti hali ya mifadhaiko na majonzi

Dalili za Presha

Kuumwa kwa kichwa

Uchovu

Matatizo ya macho

Hali ya kichefuchefu na kutapika

Hali ya woga

Hali ya kuchaganyikiwa

Kupauka kwa ngozi au kuongezeka wekundu wa ngozi
KAMA UNATATIZO HILI BASI LIMEKWISHA WASILIANA NA 0713354389/ +255752133700 UPATE USHAURI NA MATIBABU USIJALI.PRESHA INATIBIKA.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine