Pichani juu: Miss Temeke 2011 Husna Twalib (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Cynthia Kimasha (Kushoto) na mshindi wa tatu Mwajabu Juma mara baada ya kutangazwa matokeo.
MREMBO Husna Twalib, usiku wa kuamkia leo aliibuka na kutwaa taji la Miss Temeke 2011 katika kinyang’anyiro kilichofanyika ukumbi wa TCC Club uliopo Changombe jijini Dar es Salaam ambapo Cynthia Kimasha alishika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mwajabu Juma. Washindi hao watatu wamepata nafasi ya kujiunga katika kambi ya Miss Vodacom Tanzania ambayo inatarajiwa kuanza mwanzoni wa mwezi Agosti mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment