WAKATI siku za kuwasilisha majina kwa ajili ya usajili zikifikia tamati, watani wa jadi Simba na Yanga wamefanya mambo kadhaa ambayo hayakutarajiwa.
Yanga na Simba wamewasilisha majina yao kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa ajili ya msimu mpya wa 2011/12 huku baadhi wakiingia katika hatua za mwisho.
Simba imefanya usajili wa wachezaji watatu mwisho ambao ni mshambuliaji Felix Sunzu raia wa Zambia, beki Victor Costa, Mtanzania aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Msumbiji na kipa kinda,Wiliam Mweta kutoka Toto Afrika.Ukiachana na hivyo, watani wake
Yanga wamewasilisha majina ya wachezaji watatu wa kigeni na nane wanaotokea hapa nyumbani kwa ajili ya usajili mpya.
Simba imewasilisha wanne wageni.Usajili wa Oscar Joshua kutoka Ruvu Shooting unaweza kuisumbua Yanga kutokana na kupelekwa barua mbili tofauti TFF, moja ikimruhusu na moja ikipinga usajili wake kwenda Jangwani.Presha ilikuwa juu mwisho hasa kwa Simba ambayo haikuwa imekamilisha usajili tofauti na Yanga ambayo ilisajili wachezaji wake mapema na asilimia kubwa walishiriki michuano ya Kagame na kufanikiwa kuipa ubingwa.Ifuatayo ni idadi kamili ya wachezaji waliosajiliwa kutoka hapa nyumbani na nje ya nchi lakini pia wale waliopelekwa kwa mkopo.
Yanga:Majina nyumbani:Oscar Joshua (Ruvu Shooting), Godfrey Taita (Kagera), Julius Mrope, Shaaban Kado (Mtibwa Sugar), Said Mohamed (Majimaji), Pius Kisambale (JKT), Rashid Gumbo (Huru) na Idrissa Rashid (Africa Lyon).Majina wageni:Haruna Niyonzima (APR), Kenneth Asamoah (IF Jagodina) na Hamis Kiiza (URA).Waliotolewa kwa mkopo:Tonny Ndollo (Toto Afrika), Omega Seme, Salum Telela (Moro United) na Idd Mbaga (African Lyon).
SIMBA:Majina nyumbani:Mwinyi Kazimoto (JKT), Salum Machaku, Obadia Mungusa (Mtibwa Sugar), Said Nassor (Oljoro), Victor Costa (Gasabre), Mweta (Toto), Kapombe, Ulimboka Mwakingwe (Majimaji) na Haruna Moshi (Gefle IF).Majina wageni:Felix Sunzu (Al Hilal), Derreck Walulya (URA), Kago (Afrika ya Kati) na Mutesa Mafisango (Azam FC).kwenda kwa mkopo:Mohammed Banka, Mohammed Kijuso, Shamte Ramadhani (Villa Squad), Salum Gilla (Coastal Union) Meshack Abel (Ruvu Shooting), Juma Jabu, Paulo Terry, Geofrey Wambura na Adrew Kazembe (Moro United),
0 comments:
Post a Comment