Mlezi na mshauri mkuu wa bendi ya taarab ya Mashauzi Classic, Juma Mbizo akiwakaribisha waandishi wa habari (hawapo) pichani. Kiongozi wa bendi hiyo, Aisha Mashauzi akizungumza na waandishi.MWIMBAJI nyota wa miondoko ya pwani wa Bendi ya Jahazi Molden Taarab, Aisha Ramadhani Makongo ‘Isha Mashauzi’, ametangaza kujitoa rasmi katika kundi hilo la Jahazi ili kuliendeleza kundi lake la Mashauzi Classic Molden Taarab.Akizungumza na waandishi wa habari hii, makao makuu ya bendi hiyo yaliopo Kinondoni Mkwajuni, Aisha alitangaza kulizindua rasmi kundi lake hilo baada ya kupata usajili na akasema litakuwa likitoa burudani kama kawaida katika kumbi mbalimbali jijini Dar na mikoa yote Tanzania. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika utambulisho huo. Thabiti Abdul (kushoto), mwanamuziki wa bendi hiyo akiteta jambo na Juma Mbizo. Bi. Hussen Jumbe akiteta jambo na mwanamuziki wa bendi hiyo Rukia Juma.
0 comments:
Post a Comment