Monday, August 22, 2011

SIMBA YAUA ARUSHA, YANGA YALALA KWA JKT RUVU.


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania imeendelea leo katika viwanja viwili tofauti ambapo timu ya Simba imeibuka kidedea, baada ya kuikandamiza timu ya Oljoro kutoka mkoani Arusha magoli 2-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kujipatia pointi tatu za awali, katika mchezo wake wa kwanza wa ligi hiyo. Timu ya Simba imejipatia magoli yake kupitia kwa wachezaji wake wa kulipwa Patrick Mafisango na Emmanuel Okwi waliofunga magoli katika kipindi cha kwanza vja mchezo huo. Watani wao wa jadi timu ya Yanga wao walikutana na timu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Maorogoro ambapo timu ya Yanga imeangukia pua baada ya kupigwa goli 1-0 na timu ya JKT Ruvu wanajeshi wa kweli.   
 

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Uplink Servers Technology | Bloggerized by Kwetu Bongo Online Magazine