skip to main |
skip to sidebar

5/16/2012 06:23:00 AM

Unknown
No comments

Mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14
kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini
ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka huu.
Vituo vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto
wasiopungua 176 na tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini
mng’amua vipaji (scout) kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu
saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana).
Vingine ni Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi),
Makongo, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam (Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana).
Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar
katika nchi 16 duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo
vingine ni Kigamboni, Tandika, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na
Tabata.
Watoto watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato
mwingine kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini
Nairobi, Kenya.
Watakaofuzu kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza
vipaji (centre of excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina
vituo viwili vya kuendeleza vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar,
Senegal.
0 comments:
Post a Comment