skip to main |
skip to sidebar

5/16/2012 06:27:00 AM

Unknown
No comments
Msimamizi wa vipindi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mwanga
Kirahi akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada iliyohusu
Teknolojia ya kisasa (Digital) Katika Utengenezaji Filamu kwenye
Jukwaa la Sanaa la BASATA wiki hii.Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Matukio BASATA, Malimi Mashili.
Mkongwe wa Muziki wa dansi Mzee Kassim Mapili akionesha manjonjo
yake baada ya kufurahishwa na mada kuhusu Mfumo Digital
iliyowasilishwa kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.
Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma Ngalimecha Ngahyoma
akichangia mada hiyo kwenye Jukwaa la Sanaa. Alishauri Wasanii
kujipanga katika kuukabili mfumo wa Digital.

Sehemuya Wadau wa Jukwaa la Sanaa waliohudhuria mjadala huo wakifuatilia
kwa makini.
Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wameshauriwakujipanga katika kutumia fursa na changamoto
mbalimbali zitakazojitokeza wakatiUlimwengu ukijiandaa kuingia kwenye
mfumo wa digital kutoka ule wa nalogia ifikapo mwaka 2014.
Ushauri huo umetolewa wikihii na Msimazi wa Vipindi vya televisheni wa
Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC) Mwanga Kirahi wakati akiwasilisha
mada iliyohusu Teknolojia ya kisasaKatika Utengenezaji Filamu kwenye
Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makaomakuu ya BASATA Ilala
Sharif Shamba.
Alisema kuwa kuhama kutokamfumo wa analogia kwenda digitali kutazalisha
fursa mbalimbali za kuendelezaSanaa nchini lakini pia ni mwanzo wa
kuibuka kwa changamto nyingi ambazo kamawasanii hawatakuwa makini basi
wanaweza kupotea na kushindwa kushindanaipasavyo.
“Mfumo wa digitali utaletaushindani katika kuandaa programu za
televisheni, utazalisha fursa kwa kazi zawasaniii wetu kuonekana
ulimwengu mzima lakini unaweza kuwa mwanzo wa kufa kwaubunifu kama
wasanii watategemea vifaa vya kisasa tu pasipo kuingiza ubunifubinafsi”
alisisitiza.
Katika hili aliwashauriwasanii kutengeneza kazi zenye ubora na zisizo za
kunakiri kutoka kwa wengine lakinipia zenye ubunifu binafsi pasipo
kutegemea vifaa hivi vya kisasa pekee kwanikinyume chake ni kukataliwa
kwa kazi zao na hatimaye kupwaya.
“Digital maana yake ni kaziza Wasanii wetu kuonekana Ulimwengu mzima,
sasa kama zitakuwa za kunakirikutoka kwa wengine na kutegemea vifaa hivi
vya kisasa tu pasipo ubunifu binafsihatutafanikiwa. Haya pekee
yanazifanya kazi zetu zisivume muda mrefu kwanizinakuwa si original
(halisi)i” alizidi kusisitiza.
Aliongeza kuwa, wasaniihawana budi kubadilika sasa na kuacha tabia ya
wao kufanya kila kitu kikuanzia umeneja, utunzi, uongozaji (directing),
uzalishaji (producing) nakadhalika kwani kwa kufanya hivyo kunazifanya
kazi zao kuwa na radha moja pekeeambayo haiwezi kudumu muda mrefu.
Wadau wengi waliofikakupata elimu hiyo kupitia programu ya Jukwaa la
Sanaa waliiomba Mamlaka yaMawasiliano nchini (TCRA) kupanga kukutana na
wasanii ili kuwapa elimu juu yamchakato wa kuhama kutoka mfumo wa
analogia kwenda digital
0 comments:
Post a Comment