Basi lenye namba za usajiri T 820 BEY
mali ya kampuni ya Muro Investment lililokuwa likitokea Tabora kuja
jijini Dar es salaam limeteketea kwa moto maeneo ya maseyu Mkoani
Morogoro majira ya saa moja usiku wa tarehe 8 may. Basi hilo lililokuwa
na abiria 65 lilipata hitilafu kwenye mfumo wake wa umeme uliosababisha
shoti iliyoanzisha moto maeneo ya uvungu wa gari hilo, ambapo lilipofika
eneo la tukio wananchi waliokuwa chini
waliweza kuliona na kupiga kelele ambapo dereva alisimamisha gari hilo,
hakuna aliyejeruhiwa wala kufariki kwani abiria wote waliweza kushuka
salama baada ya gari hilo kusimama lakini mizigo na mali zote ndani ya
gari hilo ziliteketea kwa moto.
0 comments:
Post a Comment