WAKATI kukiwemo na taarifa za baadhi ya wachezaji nyota wa klabu ya
Yanga kutemwa, mshambuliaji wa timu hiyo Jerry Tegete anadaiwa kusaini
mkataba wa kuichezea Simba katika msimu ujao wa ligi na michuano ya
kimataifa.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam, zinaeleza kuwa Tegete ambaye
ni mmoja ya wachezaji waliopigiwa mstari katika klabu ya Yanga amefikia
uamuzi baada ya mkataba wake kumalizika huku kukiwa na uwezekano mdogo
wa kuongezewa mkataba.
Hivi karibuni hali ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya
Janwani na Twiga imeonekana kubwa tete baada ya timu hiyo kupoteza
mwelekeo na hatimaye kuutema ubingwa wake uliokwenda kwa mahasimu wao wa
jadi nchini Simba.
Kama hiyoi haitoshi mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya Yanga kuchapwa
mabao 5-0 na Simba katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania
Bara ambapo Yanga ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42,
nyuma ya Azam iliyomaliza ikiwa na pointi 56 na Simba iliyomaliza ikiwa
na pointi 62.
Kwa mantiki hiyo, uongozi umepanga kukisafisha kikosi chake hivyo baadhi
ya wachezaji kuwa hatarini kutemwa kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo kushuka kiwango, nidhamu mbovu wakiwemo Tegete, Shamte Ally,
Chacha Marwa, Mohamed Mbegu, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Kigi Makasi,
Shadrack Nsajigwa na Athuman Idd 'Chuji'.
Tegete anahusishwa kwenda Simba, wakati Nsajigwa anatuhumiwa kucheza
chini ya kiwango katika mechi yao dhidi ya Simba, ambapo alisababisha
penalti mbili kati ya tatu na kuwapa mahasimu wao ushindi wa mabao 5-0,
wachezaji wengine wakiwa wamemaliza mikataba yao, ingawa ndani yake
Chuji huenda akaongezwa mkataba.
Hata hivyo wachezaji kama Nurdin Bakari, Hamis Kiiza, Kenneth Asamoah
bado wana mkataba wa mwaka mmoja, wakati Yaw Berko na Davis Mwape
mikataba yao itamalizika Novemba mwaka huu na uongozi umeshaanza
kuzungumza na kuzungumza na Berko kuangalia uwezekano wa kuongeza
mkataba wake, lakini Mwape hatacheza Yanga msimu ujao mara baada ya
mkataba wake kumalizika.
0 comments:
Post a Comment